The Orange concert yafikisha Mil.400+

Usiku wa kuamkia leo imefanyika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Watu wenye matatizo ya kusikia ambapo Viongozi mbalimbali na Wasanii maarufu wametoa michango yao iliyofikia zaidi ya Tsh. Milioni 400, Waziri Mkuu Kasim Majaliwa alipiga simu na kuahidi kuchangia Milioni 10, Mkurugenzi wa Biashara Clouds FM Sheba Kusaga na Mkurugenzi wa TVE na EFM Majizo kwa niaba ya CMG na EFM wamechangia Milioni 200 na Joseph Kusaga pekee yake amechangia Milioni 5. Waziri Mkuu Majaliwa amempongeza Mtangazaji wa Clouds FM ambaye pia ni Mkurugenzi na Muanzilishi wa Taasisi ya Dada Hood ambayo imeandaa Tamasha hilo, @mamybabytz “Naiona hii Live ikiwa Clouds TV ya Mtu maarufu Mamy Baby, nimpongeze sana, leo hii nimefarijika kuona kundi kubwa la Wasanii wetu maarufu nchini, kwa kuunga mkono na Mimi naungana nanyi, naomba nitoe mchango wangu wa Milioni 10, tupo tayari kuunga mkono jitihada hizi zinazofanywa na Mamy Baby” Wengine waliochangia ni Seba Maganga Milioni 1.5, Faudhia wa Clouds Milioni 1, DJ Fetty Laki 5 na Bravado Group wamechangia Tsh. Milioni 4 Kwa upande wa Wasanii waliochangia ni pamoja na Shilole aliyetoa Laki 5, Quick Rocka ametoa Milioni 1, Facy Masauti Milioni 2, Wema na Whozu Milioni 5, Marioo Milioni 5 .

Post a Comment

0 Comments