Naibu Waziri Mwana FA atolea ufafanuzi Bungeni kuhusu mirabaha ya Wasanii

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ametolea ufafanuzi wa baadhi ya hoja za wabunge baada ya mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ambapo moja ya jambo aliloligusia ni mirabaha ya wasanii. Mwinjuma amesema..’Nimewaomba COSOTA wanipe majina na idadi ya fedha wanazodai kutoka kwa wadaiwa wao sugu na wamefanya hivyo sasa nitumie bunge lako tukufu kutoa salamu kwa wale ambao ni wadaiwa sugu wa COSOTA kama wanaona kwamba kutumia kazi za sanaa ni halali yao bila kulipa hawa wasanii waliofanya kazi hizi wajiandae’- -Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo “Bunge hili litakapokwisha kwa maelekezo ya Waziri nitakwenda mwenyewe m
taani kuhakikisha tunafungia sehemu hizi na hazifanyi shughuli za sanaa bila kulipa wasanii ambao wametoa jasho na damu katika kuzitengeneza, mimi kama msanii sitakaa hapa nione wasanii wengine wanadhurumiwa na haki zao hazipatikani”-Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

Post a Comment

0 Comments