Ajali Yaua Geita

Watu saba wamefariki na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa katika ajali ya basi la abiria la Kampuni ya Sheraton lenye namba za usajili T922 ADC iliyotokea katika kijiji cha Mwilima Kata ya Kasamwa Wilayani Geita Mkoa wa Geita baada ya tairi la mbele kupasuka na basi kutumbukia Darajani. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Berthaneema Mlay amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema ajali imetokea leo jioni baada ya kupasuka kwa tairi ya mbele ya basi hilo. “Basi hilo lilikuwa likitokea Mkoani Mwanza kuelekea Ushirombo Mkoani Geita ambapo Dereva alipoteza ustahimilivu baada ya tairi ya mbele kupasuka na basi kutumbukia darajani” Kamanda Mlay amesema miili ya Marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita ambapo Majeruhi wamepelekwa katika Kituo cha Afya Kasamwa kwa huduma ya kwanza na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa matibabu zaidi. #CleverUpdate

Post a Comment

0 Comments